NADHANI kila mdau wa burudani anafahamu kwamba wiki iliyopita bendi ya EXTRA BONGO ilichota wasanii 8 toka African Stars 'Twanga Pepeta', lakini hiyo sio issue Wadau kwani Twanga Pepeta ni kitivo cha mafunzo bado inaendelea kusongesha.
Asha Baraka, Mkurugenzi wa bendi hiyo amesema kwamba hakuna lililoharribika kwani kuna vichwa vimeshaziba hivyo mambo yanakwenda kama kawaida.
Ukitaka kuhakikisha maneno ya Asha jongea mjengoni (bilicanas)usiku wa leo ujionee, kama ukishindwa ibukia katika maonyesho yake mengine.
Post a Comment