YANGA ya Dar es Salaam imeendelea kusuasua katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya leo kufungwa 1-0 na Azam FC, bao pekee la John Bocco 'Adebayor'. Simba nao wameshindwa kuendeleza wimbi la ushindi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Simba imezidi kujitanua kileleni baada ya kufikisha pointi 14, wakati Yanga imebaki na pointi zake sita katika mechi sita.

1 Comments

  1. EEH!WAMEFUKIA MAITI NYINGINE NINI?YANGA MWAKA HUU INAFUNGWA MPAKA NA AZAM AMBAO MARA NYINGI HUWASUMBUA WANYAMA....HII KALI,SINA LA KUSEMA

    ReplyDelete

Post a Comment

Previous Post Next Post