YANGA ya Dar es Salaam leo kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Wakati hali ikiwa hivyo kwao, wapinzani wao wa jadi, Simba SC leo wamepanda kileleni mwa ligi hiyo, baada ya kuifunga Villa Squad 1-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, bao pekee la mshambuliaji wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Gervais Kago. Yanga sasa wapo kwenye wakati mgumu, kwani hiyo inakuwa mechi ya tatu katika Ligi wanatoka uwanjani vichwa chini, baada ya awali kufungwa 1-0 na JKT Ruvu, baadaye kulazimishwa sare ya 1-1 na Moro United, mechi zote wakipiga kwenye Uwanja huo. Kabla ya Ligi, Yanga ilifungwa mara mbili 3-1 kila mechi na El Hilal ya Sudan mjini Khartoum baadaye ikapigwa 2-0 na Simba SC katika mechi ya Ngao ya Jamii mjini Dar es Salaam. kunani Yanga? watajijyuuuuuu. Ndio faida ya migogoro hiyo.

MTOTO MBAYA WEWE..LEO NDIO UMEAMUA KABISA KUDHIHIRISHA USIMBA WAKO,ETI WATAJIJU,HAYA BWANA NYIE TANGULIENI TU NA HIYO BAISKELI YENU YA MITI KAMA LAST SEASON,TUNAJUA PA KUWAKAMATA.....
ReplyDeletePost a Comment