MCHEZO wa marudiano wa kombe
la Shirikisho baina ya Azam Fc na Al Nasir Juba ya Sudan Kusini unatarajiwa
kupigwa Machi 3 mwaka huu, imefahamika.
Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura
alisema kwamba, wamepokea barua kutoka chama cha soka cha nchi hiyo na kuwapa
taarifa hizo.
Alisema mchezo huo
unatarajiwa kupigwa katika dimba la Juba Stadium, huko Sudan Kusini kuanzia saa
11.30 jioni kwa saa za hapa nyumbani.
Katika mchezo wa awali
uliopigwa hapa nchini wiki iliyopita Azam ilishinda mabao 3-1, hivyo wenyeji
wanahitaji kushinda mabao 2-0 ili kusonga mbele.

Post a Comment