Na Mwandishi Wetu
WAANDISHI wa habari nchini wamehimizwa kujiunga na mfuko wa hiyari (HIFADHI SCHEME) unaotolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii (NSSF) ili kujiwekea Kinga ya kesho yao.
Wito huo umetolewa na Mweka Hazina wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) CPE Dk.James Kalanje wanachama wa cha Wafanyakazi kwenye Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA).
Alisema sekta ya habari ni mhimili mkuu wa demokrasia, uwazi, uwajibikaji na maendeleo ya nchi.
"Nyinyi ni kioo cha jamii, makocha wa fikra za wananchi, na sauti ya wanyonge. Mnafanya kazi usiku na mchana, kwenye jua na mvua, bila kujali hatari zinazowakabili, ili kuhakikisha taifa linapata taarifa sahihi kwa wakati",alisema
Kalanje aliongeza kuwa inasikitisha kuona kwamba licha ya mchango wao mkubwa kwa taifa, wengi waliopo katika sekta hiyo hasa wale wa kujitegemea na binafsi wanaishi bila kuwa na kinga rasmi ya kesho yao.
"Maisha ya mwandishi wa habari kama yalivyo maisha ya mfanyakazi mwingine yeyote, hayana budi kupangiliwa kwa umakini mkubwa. Takwimu zisizo rasmi zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya waandishi wa habari hawapo kwenye mfumo wa hifadhi ya jamii",Aliongeza
Hii ina maana gani? Ina maana kuwa siku nguvu zikiisha, au pale ambapo mwanahabari atakumbwa na janga la ghafla kama kuugua au kupoteza uwezo wa kufanya kazi, maisha hugeuka kuwa mlima mgumu kuupanda. matokeo yake yanakuwa ni kuanza kutanga tanga na kuomba msaada kwa ndugu, jamaa na marafiki, jambo ambalo haliendani na heshima ya jasho mnalolitoa kwa taifa hili,"alisema
Aidha,Kalanje aliipongeza NSSF kwa ubunifu na mwendelezo wa kutoa elimu inayolenga kugusa moja kwa moja mustakabali wa maisha ya wafanyakazi kwani Hifadhi Scheme unawapa fursa ya kipekee wafanyakazi wa sekta binafsi na wale waliojiajiri wenyewe kujiwekea akiba kidogo kidogo kwa kadri ya uwezo wao.
"Hii sio tu kwamba inajenga mtaji wa uhakika wa kipato cha uzeeni, bali pia inawalinda dhidi ya dhoruba za kiuchumi na pia mbali na akiba ya uzeeni, mwanachama anapata fursa ya bima ya matibabu",Alisisitiza
Kalanje alitoa wito kwa waajiri wa vyombo vya habari kuhakikisha wanaweka mazingira rafiki yatakayowezesha au kuwahamasisha hifadhi ya jamii huku akiwasihi NSSF kuhakikisha wanatanua wigo zaidi na zaidi ili kuwafikia waandishi na wananchi wote waliopo katika sekta isiyo rasmi nchi nzima, ili kujenga kesho ilioyo bora kwa kila Mtanzania.

Post a Comment